Ruhusu amani yake, Kataa mahangaiko
Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. – Yohana 14: 27
Bwana Yesu ni Mfalme wa Amani, yuko ndani mwetu kwa njia ya Roho wake, hivyo basi tunayo amani yake ndani mwetu! Tusimruhusu ibilisi atuibie amani hiyo, tusiyaruhusu masumbufu ya maisha haya yatupore amani tuliyonayo ndani ya Yesu.
Labda unajiuliza, ninafanyaje kuzuia amani ya Mungu isiondoke ndani mwangu? Jibu ni kuliamini Neno la Mungu linavyosema na kulishika. Mfano, Baba yako wa Mbinguni anasema, “sitakuacha wala sitakupungukia”, unalishika Neno hilo unalitafakari, yakikujia mawazo (toka kwa yule adui) kama “Mungu amekuacha au Mungu hana mpango na wewe” badala ya kuyapokea unayakataa na kuendelea kukiri ahadi ya Mungu kwamba hatakuacha wala kukupungukia. Amani yake itaendelea kutawala moyoni mwako.
Usifadhaike moyoni mwako wala usiwe na woga kwani amani yake imo ndani mwako, na tayari unao uwezo wa kukataa hofu na mahangaiko yoyote yatakayojaribu kukuibia amani hiyo.
Iruhusu amani yake itawale katika kila eneo la maisha yako leo! Mbarikiwe sana!
Blessings,
Patrick
You must be logged in to post a comment Login