Adui kukuletea uongo unaoangamiza ila unaonekana kama unahitajika
Shetani ni Mwongo. Usimwamini, Kamwe usiamini neno toka kwa Shetani. Maneno ya Yesu mwenyewe juu ya Shetani na uongo wake alisema “Ninyi ni watoto wa baba yenu Ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.”Yohana 8:44 (Biblica version)
Wangapi wamewahi kusema uongo? Ulianza kusema uongo ukiwa na umri gani? Unaposema uongo unakuwa unataka kupata vitu kwa njia isiyo halali? Unasema uongo unapotafuta mwenzi wa maisha, kazi, masomo, biashara na nini tena? Uko tayari kuibia wengine kupata kitakachokufurahisha wewe kwa uongo?
Kama unafanya hivi iko damu ya adui, iko mbegu ya adui maishani mwako.iko roho ya adui inafanya kazi kwako Nimetaja damu sababu kuna wana wa ibilisi. Nimetaja mbegu kwa maana ya DNA ya adui. Matokeo ya madhara yake ni makubwa….Na unapodhani kwamba utadanganya na kukwepa bila kushikwa ndivyo unavyodanganyika zaidi… Isaya 15-18 Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti, tumefanya mapatano na kuzimu. Wakati pigo lifurikalo litakapopita, haliwezi kutugusa sisi, kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio
letu na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.’’ 16Kwa hiyo hivi ndivyo BWANA Mwenyezi asemavyo:
“Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembe la thamani kwa ajili ya msingi thabiti, yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu. 17Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia na uadilifu kuwa timazi, mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo, nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha. 18Agano lenu na kifo litabatilishwa, patano lenu na kuzimu halitasimama. Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba litawaangusha chini.(version ya biblica)
Jitahidi sana kuelewa umuhimu wa kweli na uadilifu…
Usijifunze uongo jifunze kweli, usitegeemee uongo tegemea kweli, panda uadilifu, jifunze uadilifu na uwe mwadilifu. Uwe kama Mungu wetu ambaye hawezi kusema uongo Waebrania 6: 18 Mungu alifanya hivyo, ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi Yake na kiapo Chake, ambavyo kwa hivyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia, tuwe na moyo mkuu kulishika lile tumaini lililowekwa mbele yetu. (Biblica version)
Ukimaliza kusoma hii waweza kumwomba msamaha Mungu kwa kusema na kutenda uongo, na kuomba msamaha kwa wale unaolazimika kuwaomba msamaha kwa kuwadnganya kadri utakavyoweza.
Kumbuka kama ambavyo hupendi kudanganywa usidanganye wengine…
Wako Abel na Rebecca Orgenes – “B” family ministry!
You must be logged in to post a comment Login